Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Goran aamua kubaki Tabora United

Goran Kopunovic (1) Goran aamua kubaki Tabora United

Mon, 1 Jan 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Ile hofu waliyokuwa nayo mashabiki na wapenzi wa Tabora United kukimbiwa na kocha wa timu hiyo, Goran Kopunovic, imeisha baada ya kocha huyo kuamua kusalia kwenye kikosi hicho akizima uvumi wa kutaka kutimka kwa madai ya kutolipwa mishahara wa miezi miwili.

Mbali na uvumi wa Goran kutaka kusepa kwa ishu ya mshahara, pia ilidaiwa alikuwa na ofa tatu mezani zilizomchanganya, lakini habari kutoka klabuni hapo zinasema kocha huyo amegeuza mpango baada ya kumalizana na mabosi wa klabu hiyo.

Tabora iliyopanda daraja na kuanza kuchezea Ligi Kuu msimu huu, haijawahi kubadilisha kocha mpaka sasa, huku ikishikilia nafasi ya 12 katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 15.

Akizungumza na Mwanaspoti, Goran alisema aliamua kuzikacha ofa zote kutokana na malengo makubwa waliyonayo wachezaji na uongozi kwa ujumla pamoja na upendo wa dhati alionao kwa timu hiyo.

Aidha, alieleza kuwa nje na malengo kwake haikuwa rahisi kuanza kufundisha timu nyingine, kwani kila kitu huwa kinaanza upya na kuchukua muda mrefu kutambua uwezo wa kila mchezaji na namna ya kupanga kikosi.

“Kwa sasa nimeona nibaki na akili moja, hapa Tabora United tuna mradi wa kuufanikisha pamoja, lakini sitaacha kuzishukuru klabu zote zilizotaka kunipa kazi ila naona bado nina deni hapa,” alisema Goran ambaye ni kocha wa zamani wa Simba.

“Nimefikiria kama nitaondoka sasa nitawavunja nguvu wachezaji wangu na mashabiki wa Tabora United, pia huko nitakapokwenda nitahitaji muda kujenga uimara kama ambavyo tulijenga hapa Tabora, ni vyema uamuzi tofauti na huu kuufanya mwisho wa msimu kama nitaona kuna ulazima wa kufanya hivyo.”

Chanzo: Mwanaspoti