Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gor Mahia yatishia kuipeleka Simba Fifa kisa Tuyisenge

50298 Pic+gormahia

Thu, 4 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Nairobi, Kenya. Mabingwa wa Ligi Kuu Kenya, Gor Mahia amepiga habari za mshambuliaji wao Jacques Tuyisenge kujiunga na mabingwa wa Tanzania Bara, Simba SC.

Taarifa zimedai juzi Jumatatu kuwa mshambuliaji huyo Mnyarwanda tayari ametua Dar es Salaa na kusaini mkataba wa awali na Simba.

Inadaiwa kuwa Tuyisenge ameshawishiwa kujianga na Simba na mshambuliaji mwenzake wa zamani wa K'Ogalo, Meddie Kagere ambaye kwa sasa anatikisa katika soka la Tanzania.

Hata hivyo, Mkurungezi Mtendaji wa Gor Mahia, Omondi Aduda amepiga madai hayo akisisitiza kuwa mchezaji huyo kwa sasa yupo na timu Kisumu na hatahakisha nyota huyo anaongoza mkataba wa kubaki na vinara hao wa Ligi Kuu Kenya (KPL).

“Tuyisenge bado yupo kwenye mkataba na Gor Mahia hadi mwaka 2020 na hizo taarifa za kutakiwa haziwezi kutuchanganya. Ni mchezaji wetu na klabu yoyote inayomtaka iwe Simba au AS Vita wanaotaka kumsajili wanatakiwa wazungumze na sisi kwanza kabla ya mchezaji," Aduda aliimbia Goal.Com.

“Sheria za Fifa zipo wazi kabisa kuhusu uhamisho wa wachezaji unavyotakiwa kufanywa. Klabu inayotaka kumsajili ni lazima kuzungumza na klabu yake kwanza kabla ya mchezaji mwenyewe.

“Kama klabu yoyote haitofuata utaratibu kwa kuzungumza na mchezaji wetu basi wajiandae kuwa tutawapeleka Fifa.

Uongoza wa klabu hiyo unaamini Tuyisenge atasaini mkataba mpya wakati wa majadiliano utakapofika.

Tuyisenge alifunga penalti ya ushindi dhidi ya Petro Atletico ya Angola na kuwezesha Gor Mahia kufuzu kwa robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Tuyisenge aliyenunuliwa akitokea klabu ya Polisi FC ya Rwanda, pia hivi karibuni amehusishwa na kutakiwa na AS Vita Club ya DR Congo.



Chanzo: mwananchi.co.tz