Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gor Mahia yatinga 16 Bora

Gor Mahia Vs Kibera Gor Mahia yatinga 16 Bora

Mon, 6 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Gor Mahia imetinga hatua ya 16 bora ya Kombe la Mozzart Bet baada ya kushinda bao 1-0 dhidi ya timu ya daraja la pili ya Kibera Soccer mchezo uliochezwa uwanja wa Kimataifa wa Moi jana Jumapili.

Ukiwa ni mchezo wa hatua ya 32 wa mashindano hayo, Gor Mahia walipata bao pekee kupitia kwa mchezaji wa akiba Lloyd Khavuchi aliyekwamisha mpira nyavuni kunako dakika ya 27.

Kufuatia matokeo hayo, K’Ogalo watacheza na Kakamega Homeboyz hatua ya 16 bora ambapo kocha wa timu hiyo akizungumza baada ya mchezo huo amesema licha ya mabadiliko ya wachezaji ambao wamefanya bado wamepata walichokuwa wanahitaji.

“Mchezo umeenda kama tulivyopanga, tulihitaji kufuzu kwenda hatua inayofuata. Sisi ni mabingwa watetezi tunahitaji kutetea kwa mara nyingine tena”, alisema Johnathan McKinstry, kocha wa Gor Mahia.

Kakamega Homeboyz mapema walishinda kwa penati bao 3-4 kwa Shalimar, Sofapaka wametinga pia hatua hiyo kwa kushinda 3-0 dhidi ya Karatina.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live