1. Simba wamekosa namna ya kudhibiti maadui wasiingie kwenye himaya yao. Himaya ya Simba imekuwa ikiingiliwa kirahisi na maadui. Maadui wanaingia kirahisi ndani ya ngome ya Simba na kutengeneza mtandao.
2. Mtu aliyekuwa anaweza kuzuia maadui wasiisogelee ngome ya Simba kirahisi na kutengeneza mtandao tayari ametangulia mbele ya haki, marehemu Zacharia Hans Poppe.
Hans Poppe aliweza kuzuia maadui wasiingie ndani ya Simba na kuwadhuru kwa sababu yeye mwenyewe alikuwa anajimudu kiuchumi. Kwa hiyo kwenye vita alikuwa anapambana hata kwa kuweka fedha zake ili kuzuia maadui wasiingie.
3. Sasa hivi maadui wanaingia kirahisi kwenye ngome ya Simba na kutengeneza mtandao, wanafanya wanalolitala. Kwa hiyo Simba wanapambana kujipata wakati maadui wanakitafuta wanachokitaka!
4. Maadui wana nguvu kubwa kiuchumi kuingia ndani ya Simba na kuwavuruga kwakuwa kwa sasa hakuna mtu mwenye nguvu ya kuwazuia wasiingie.
5. Mwenye dhamira ya kuwekeza Simba anawagawanya ili ionekane bila yeye Simba haiwezi kufanya chochote!
Mwaka 2018 thamani ya Simba ilikuwa ni Tsh. 20 bilioni. Je, leo thamani ya Simba bado ni Tsh. 20 bilioni?