Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gomes awapa tano wachezaji

6c1fa89a82fc6a9be892e907962bbafc Gomes awapa tano wachezaji

Sun, 14 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

KOCHA Mkuu wa Simba, Didier Gomes amesema anajivunia kiwango bora kilichooneshwa na wachezaji wake katika mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya AS Vita akisema ni mwanzo mzuri.

Katika mchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja wa Martyrs Kinshasa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, juzi Simba iliibuka na ushindi wa bao 1-0 ikiwa ni ushindi wa kwanza kupata ugenini tangu wafike hatua hiyo

Akizungumza baada ya mchezo huo Gomes alisema amefurahishwa na kiwango cha wachezaji wake na anajivunia kwani mbinu alizowapa zimezaa matunda.

“Nimefurahi na ninajivunia kile walichokifanya na kutuwezesha kupata pointi tatu katika mchezo wa ugenini, mbinu zetu za kujilinda na kuwaheshimu wapinzani wetu zimefanikiwa,”alisema.

Alisema waliwajua wapinzani wao mapema ni timu iko vizuri katika kushambulia wakaona ni bora kutowapa nafasi ya kupenya kwa kulinda na kuwadhibiti na kutumia nafasi pale itapopatikana.

“Tuliwajua wapinzani wetu mapema tukajipanga na niliwaeleza wachezaji wawe makini wanapopata mpira na wanapopoteza waongeza umakini kwa sababu AS Vita ni timu inayoshambulia,” alisema.

Kocha huyo alisema anajua mamilioni ya Watanzania watakuwa wanafurahia kile walichoonesha na sasa wana mpango wa kuendelea kufanya vizuri katika mechi zijazo.

Alisema kuna makosa machache yalionekana kabla ya kukutana na Al Ahly katika mchezo wa pili utakaochezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa Februari 23, mwaka huu basi wanahitaji kurekebisha.

Aidha alisema kwa sasa anahitaji kuisoma Al Ahly kwani wamefanya vizuri katika mashindano ya klabu bingwa ya dunia kwa kushika nafasi ya tatu.

Katika hatua nyingine, Balozi wa Tanzania nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Luteni Jenerali mstaafu,Paul Mella aliwapongeza Simba kwa kupata matokeo mazuri.

Akizungumza nao baada ya ushindi huo Mella alisema “ kwa ushindi huu mmeiweka nchi yetu mahali pazuri, ni heshima kubwa na nyumbani wanawangojeeni,”.

Chanzo: habarileo.co.tz