Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gomes amuanzisha Mkude, Simba ikiwakabili African Lyon

Mkude Nomapic Data Gomes amuanzisha Mkude, Simba ikiwakabili African Lyon

Sun, 28 Feb 2021 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By Ramadhan EliasMore by this Author ZIKIWA zimesalia dakika chache kuanza kwa mchezo wa michuano Azam Sports Federation Cup (ASFC) kati ya Simba na African Lyon tayari vikosi vya timu zote mbili vitakavyocheza leo vimewekwa hadharani.

Simba ambao ni wageni katika mchezo huo wameonekana kufanya mabadiliko katika kikosi chao cha leo katika maeneo matatu kwa maana ya Beki, kiungo na Ushambuliaji.

Upande wa beki wa kulia ambao kwa mchezo uliopita dhidi ya Al Ahly alipangwa Shomari Kapombe, leo hii ataanza Kennedy Juma huku koshoto alikozoeleka kucheza Mohammed Hussein ataanza Gadiel Michael.

Erasto Nyoni na Ibrahim Ame wanatarajiwa kucheza eneo la beki wa kati ambalo mchezo ulopita walicheza Paschal Wawa na Joash Onyango.

Katikati ya uwanja kwa maana ya kiungo, kocha mkuu wa timu hiyo Didier Gomes amemuanzisha Jonas Mkude ambaye kwa muda mrefu hajaonekana uwanjani kutokana na kusimamishwa kwa makosa ya kinidhamu ambayo hata hivyo yalitatuliwa.

Ibrahim Ajib pia ataanza leo sambamba na Rally Bwalya huku Taddeo Lwanga na Mzamiru Yassin walioanza kwenye mechi iliyopita dhidi ya Ahly wakipumzishwa.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz