Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gomes amtega Mkude Simba

Onyango Pic Data Gomes amtega Mkude Simba

Thu, 4 Feb 2021 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By Thobias SebastianMore by this Author KIKOSI cha Simba jioni ya leo kitashuka Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma kula kiporo cha Ligi Kuu Bara dhidi ya Dodoma Jiji, huku Kocha Mkuu wa timu hiyo, Didier Gomes akimruhusu kiungo mkabaji wake, Jonas Mkude kuanza tizi na wenzake kwa masharti maalumu.

Mkude alikuwa amesimamishwa kwa muda wa kama mwezi mmoja uliopita kwa utovu wa nidhamu, lakini Kamati ya Nidhamu iliamua kumpiga faini ya Sh2 milioni na kumfungulia, na kocha Gomes naye amemruhusu kujiunga mazoezini, lakini baada ya kikao kizito na nyota wenzake, kisha akatoa masharti kwa kiungo huyo na mwingine kuwa wakijichanganya wajue inakula kwao mazima.

Mchana wa Jumanne kabla ya kwenda mazoezini kulikuwa na kikao kizito kati ya Ofisa Mtendaji Mkuu, Barbara Gonzalez, benchi la ufundi lililoongozwa na Gomes na wachezaji kujadili kurejea tena kikosini Mkude.

Katika kikao hicho wachezaji walionekana kuleta ugumu kwa madai ya kutaka zipite kwanza mechi 10 ndipo Mkude ajiunge na wenzake katika mazoezi na ratiba nyingine za timu ambazo zinaendelea kila siku.

Baada ya mvutano na majadiliano ya huku na kule, Gomes aliwaambia wachezaji kuwa tukio la Mkude lilitokea wakati timu haipo chini yake, hivyo wachezaji wanatakiwa kusahau ya nyuma na kumsamehe mwenzao arudi kambini.

Gomes baada ya kauli hiyo aliwaeleza wachezaji kuanza upya na atakuwa muumini wa kusimamia nidhamu kwenye maeneo yote na kama akitokea mmojawapo amekwenda tofauti bila ya sababu atakutana na adhabu.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz