Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gomes aifurahia Kaizer Chiefs

Ae4be9979d2857df8a9f90d12d498ee0.jpeg Gomes aifurahia Kaizer Chiefs

Sun, 2 May 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

KOCHA Mkuu wa Simba, Didier Gomes amesema kuwa amefurahi kupangiwa Kaizer Chiefs katika ratiba ya robo fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa wa Afrika.

Shirikisho la Soka Afrika (Caf) juzi Ijumaa lilipanga ratiba ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa na ile ya Kombe la Shirikisho Afrika, na Simba itaanzia ugenini dhidi ya timu hiyo ya Afrika Kusini katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa wa Afrika.

Gomes alisema kuwa wapinzani wao hao ni wazuri na kingine alichokifurahia ni kuanzia ugenini, ambapo mechi hiyo itapigwa kwenye Uwanja wa FNB uliopo katika jiji la Johannesburg, Afrika Kusini.

Kwa mujibu wa mtandao wa Caf, Gomes alisema kuwa wanacheza mchezo wa kwanza ugenini, hivyo wanatakiwa kuwa tayari kwa mpambano huo kwani utakuwa mchezo mgumu.

Alisema kuwa wanaiheshimu sana Kaizer Chiefs na lengo lao ni kufika mbali katika michuano hiyo.

Alisema Simba wako tayari kukabiliana na timu hiyo, na kama watafuzu, basi watakuwa tayari kucheza na mpinzani yeyote yule watakayekutana naye katika nusu fainali.

Alisema kuwa hatua ya robo fainali sio rahisi na baadae watafikiria kuhusu hatua inayofuata. “Nina uhakika msimu huu Simba watafika mbali.”

Naye Kocha wa Kaize Chiefs, Gavin Hunt alisema kuwa timu ya Simba watakayokutana nayo ni ngumu, na ilikuwa na wakati mzuri katika hatua ya makundi, ambako waliwafunga hata mabingwa watetezi, Al Ahly.

Alisema kuwa watakuwa makini katika kila mchezo na wakianzia mchezo huo wa nyumbani. Pia na wao walikuwa na mwenendo mzuri katika hatua ya makundi na wataendelea kuwa na kazi nzuri.

Naye Ofisa Mawasiliano wa Simba, Haji Mara alisema kuwa timu yao itacheza fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa wa Afrika.

Chanzo: www.habarileo.co.tz