Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gomes achukua hatua fasta Simba SC

Didier Gomes 2?fit=2000%2C1334&ssl=1 Kocha wa Simba, Didier Gomes

Thu, 7 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati kikosi chake kikionekana bado hakina muunganiko mzuri, Kocha Mkuu wa Simba, Didier Gomes, ameamua kuwarudisha fasta mazoezini nyota wake kujiandaa na mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Jwaneng Galaxy ya Botswana.

Gomes amelazimika kukirejesha kikosi chake mazoezi jana jioni baada ya kuwa na mapumziko ya siku mbili tayari kwa kujiandaa na mchezo huo wa hatua ya kwanza utakaochezwa Oktoba 14, mwaka huu nchini Botswana.

Taarifa kutoka ndani ya Simba, zimesema kwamba, Gomes bado hajaridhishwa na kiwango cha kikosi chake, hivyo amewataka mastaa wote ambao hawajaenda kwenye timu zao za taifa kuwasili mazoezini bila kukosa ili aweze kuwanoa kabla ya kukutana na Wabotswana hao.

“Kocha amesema kuwa tayari amewafuatilia wapinzani wetu wale Wabotswana na kuona uchezaji wao, hivyo hawezi kutoa siku za mapumziko zaidi ya mbili kwa wachezaji wake, pamoja na kwamba hawajapata muda mrefu wa kupumzika.

“Sababu kubwa ni kwamba bado haridhishwi na muunganiko wa kikosi chake na angependa kutumia muda huu kuweka sawa muunganiko huo,” kimesema chanzo hicho.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live