Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gomes abadili kikosi, Simba ikiikabili Lyon

Gomes Pic Data Gomes abadili kikosi, Simba ikiikabili Lyon

Sun, 28 Feb 2021 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By Olipa AssaMore by this Author WACHEZAJI wa Simba ambao hawakupata nafasi katika mchezo uliopita dhidi ya Al Ahly wanatarajiwa kupewa nafasi kubwa ya kuanza mechi ya leo dhidi ya African Lyon.

Simba inashuka kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa saa 1:00 jioni leo Ijumaa ya Februari 26,2021 ikiwa ni mchezo mtoano wa Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC).

Kupitia kwenye mtandao wa Simba wa kijamii (Instagram), kocha  wao Didier Gomes amesema lengo lake ni kutaka wachezaji wengine waonyeshe uwezo wao kwa mashabiki pia kuwapumzisha wale ambao walicheza dhidi ya Al Ahly.

"Tunawapa nafasi wachezaji wengine waonyeshe mashabiki kwamba wapo vizuri, pia kutoa nafasi ya kuwapumzisha wachezaji waliocheza mchezo wa Al Ahly, sababu wanahitaji kupumzika," amesema.

Amesema lengo lake ni kuona wanafanya vizuri CAF, ASFC na Ligi Kuu Bara, hivyo kila mchezaji anataka apambane kwa kadri anavyoweza kuisaidia timu kupata ushindi.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz