Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gomes: Tunataka heshima kwa Ahly

1885ef253a81dff7ea9d967bdc7bbafb Gomes: Tunataka heshima kwa Ahly

Wed, 7 Apr 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

KIKOSI cha Simba kimeondoka nchini kwenda Cairo, Misri kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly ya nchi hiyo, kikiwa na matumaini ya kwenda kuendeleza ushindi.

Kikosi hicho kiliondoka jana na wachezaji 25 kupitia Dubai kwa ajili ya mchezo huo wa mwisho wa makundi uliopangwa kuchezwa keshokutwa saa nne usiku.

Akizungumza saa chache kabla ya kuondoka nchini, kocha wa Simba, Didier Gomez alisema anataka kuweka heshima licha ya kufuzu robo fainali hivyo ameondoka na kikosi kamili kwa ajili ya mchezo huo.

“Licha ya kufuzu nataka kuweka heshima ya kutokufungwa katika hatua ya makundi ndio maana nimeondoka na nyota wote,” alisema.

Wachezaji waliondoka ni makipa Aishi Manula, Beno Kakolanya na Ally Salim, mabeki ni Shomari Kapombe, Joash Onyango, Pascal Wawa, Ibrahim Ame, Erasto Nyoni, Gadiel Michael, Mohamed Hussein, Kennedy Juma na David Kameta

Viungo ni Jonas Mkude, Rally Bwalya, Said Ndemla, Mzamiru Yassin, Luis Miquissone, Hassan Dilunga, Clatous Chama, Bernard Morrison, Francis Kahata na Thadeo Lwanga.

Washambuliaji ni Medie Kagere, John Bocco, Ibrahim Ajib na Chris Mugalu.

Simba inaongoza Kundi A ikiwa na pointi 13 ikifuatiwa na Al Ahly yenye pointi nane, AS Vita ina pointi nne na Al Merrikh ina pointi mbili.

Simba na Al Ahly zimefuzu hatua ya robo fainali kwa tofauti ya pointi tano.

Timu hizo katika michezo mitano ya mwisho kukutana, Simba imeshinda mara mbili na imefungwa mchezo mmoja, lakini michezo yote imeshinda nyumbani na mchezo wa mwisho waliocheza Misri, wenyeji Al Ahly waliifunga mabao 5-0 mwaka 2019 ndio maana Simba wanasema wanakwenda kulipa kisasi.

Chanzo: www.habarileo.co.tz