Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gomes: Tuachieni sisi hao Kaizer

Kaizer Chief Pic Data Gomes: Tuachieni sisi hao Kaizer

Mon, 17 May 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

MASHABIKI wa Simba hawajui kipi kimewatokea nchini Afrika Kusini wakipoteza vibaya dhidi ya wenyeji wao Kaizer Chiefs lakini bosi wa ufundi Gomes De Rossa ametamka mambo mazito kisha akamalizia kwa kusema: “Tuachieni sisi tunajua cha kufanya.” Simba ina mlima mrefu wa kupanda ikitakiwa kushinda kwa mabao 5-0 nyumbani kwenye Uwanja wa Mkapa ili kutinga nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya juzi kuchapwa 4-0 huko Afrika Kusini.

Akizungumza na Mwanaspoti jana, Gomes alisema matokeo hayo yametokana na wachezaji wake kufanya makosa lakini bado wana nafasi ya kubadilisha matokeo katika dakika 90 za nyumbani.

“Tumefanya makosa ambayo yamewapa matokeo wapinzani wetu, huu ni mchezo wa soka unapocheza mechi kubwa kama hii hupaswi kuwa katika ubora mdogo kama tulivyokuwa sisi,” alisema Gomes ambaye anapoteza vibaya kwa mara ya kwanza tangu atue Simba.

“Huu sio wakati wa kuangalia mechi iliyopita sasa ni wakati wa kuangalia mchezo ujao wa nyumbani, wameshinda huku lakini tuna nafasi ya kupata ushindi nyumbani.”

Gomes alisema amekutana na wachezaji wake na amewaambia kwamba watafanya masahihisho ya makosa waliyofanya ili wapate ushindi nyumbani.

“Tunatakiwa kuwa bora nyumbani kwa kutofanya makosa kama ambavyo wao walivyojipanga utakuwa ni mchezo mgumu lakini Simba bado ina nafasi.

“Nimewaambia wachezaji kwamba sisi makocha tunajua kazi ya kufanya, muhimu ni kushinda nyumbani, waache kuwaza aina ya ushindi tunatakiwa kushinda nyumbani bila kuanza kufikiria idadi ya mabao, tuna nafasi kubwa ya kuwapa kitu mashabiki wetu ambao wanatuamini zaidi. Muhimu ni kuwa na ubora na kuacha kufanya makosa kama ya jana (juzi), tulielekezana mambo ambayo hatutakiwi kuyafanya lakini ndio hayo tulikwenda kuyafanya na tumeadhibiwa,” alisema.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz