Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gomes: Safari ya ubingwa imeanza

12c04fc6292b006ac53454022842e926 Gomes: Safari ya ubingwa imeanza

Mon, 26 Apr 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

KOCHA Mkuu wa Simba, Didier Gomes amesema baada ya kukaa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu sasa anaanza rasmi safari ya ubingwa. Simba imemaliza kwa kishindo michezo yote ya Kanda ya Ziwa baada kuondoka na pointi tisa katika michezo yote mitatu na kufikisha pointi 58 ikiwa kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo.

Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, walianza kampeni yao ya Kanda ya Ziwa Shinyanga kwa kuichapa Mwadui bao 1-0, kisha wakaifuata Kagera Sugar Bukoba ambayo ilikubali kichapo cha mabao 2-0 na kuhitimisha na Gwambina FC kwa kuwalaza kwa bao 1-0, Misungwi, Mwanza.

Akizungumza na gazeti hili jana Gomes, alisema kuwa amefurahishwa na kazi kubwa iliyofanywa na wachezaji wake baada ya kutimiza malengo waliyokuwa wamejiwekea ya kupanda kileleni mwa msimamo kwa kushinda michezo minne mfululizo.

“Tumefanikiwa na kutimiza lengo letu kama timu kiu yetu ilikuwa kupanda juu ya msimamo wa ligi jambo ambalo limefanikiwa sasa rasmi tumeanza mbio za kulisaka taji la Ligi Kuu.

“Halikuwa jambo rahisi lakini wachezaji wangu wamepambana na kufanikisha hili tunashiriki mashindano mengi ambayo tunapaswa kupambana kwa nguvu na kulipa fadhila kwa mashabiki wetu ambao wamekuwa wakitusapoti bila kuchoka ,” alisema Gomes.

Naye kocha mkuu wa timu ya Gwambina FC , Mohamed Badru, alisema kuwa amefurahishwa na kiwango kilichooneshwa na wachezaji wake wamefungwa na timu bora wameadhibiwa kwa kosa moja lililofanywa na mchezaji wake baada ya kupiga pasi ya nyuma ambayo imewagharimu nyumbani.

Badru alisema kuwa wamepoteza michezo mitatu mfululizo jambo lililoharibu hesabu zao za kujiweka katika nafasi nzuri katika msimamo wa ligi lakini hawatokata tamaa wanaendelea kujipanga kwaajili ya michezo iliyosalia ya ligi.

“Unapocheza na timu bora unapaswa kuwaheshimu Simba ni timu kubwa yenye wachezaji wazuri unapocheza dhidi yao unapaswa kuwa makini sana na kupunguza makosa ili kuwakabili.

“Tumefanya kosa moja limetuhukumu nilijaribu kuufungua mchezo na kushambulia lakini walikuwa imara na katika maeneo yote naenda kuyafanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza ili tusiweze kuyarudia katika mchezo ujao wa Ligi Kuu Bara ambao tutakuwa nyumbani,” alisema Badru.

Chanzo: www.habarileo.co.tz