Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Golikipa Mtibwa Sugar bado majanga

Makaka Mohammed Makaka

Fri, 14 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amesema kuwa kuelekea kwenye mchezo wao wa jumamosi dhidi ya KMC wataendelea kumkosa kipa wao, Mohamed Makaka.

Mchezo huo wa ligi kuu Bara unatarajiwa kuchezwa Oktoba 15 mwaka huu Katika Uwanja wa Uhuru, Dar es salaam.

Kifaru amefunguka kuwa “Kwenye mchezo wetu na KMC tutamkosa Kipa wetu namba moja, Mohamed Makaka ambae hatukuanza nae msimu kutokana na majeraha aliyoyapata tukiwa kwenye maandalizi ya Ligi Kuu Bara.

“Ligi ya msimu huu ni ngumu, Kila timu inapambana ndani ya uwanja kupata alama tatu hivyo lazima kila mchezo tuingie Kwa tahadhari kubwa ili tufanikiwe kupata matokeo mazuri ambavyo ni ushindi wa alama tatu.

“Kila kitu tunamuachia Kocha Mkuu Salum Mayanga ambae naamini kuwa kwa kutumia Kikosi kipana cha timu yetu tutafanikiwa kupata alama tatu kwenye mchezo huu.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live