Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Golikipa Geita Gold atimkia Rwanda

Arakaza Pic Golikipa Geita atimkia Rwanda

Sat, 27 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Golikipa wa zamani wa Geita Gold ya Tanzania Mrundi Arakaza MacArthur amesaini mkataba wa miezi sita kwa ajili ya kuitumikia timu ya Etincelles FC inayoshiriki Ligi Kuu Rwanda.

Arakaza Mac Arthur ambaye aliitumikia timu ya Taifa ya Burundi Intamba Murugamba tangu mwaka wa 2012 kwasasa akiwa ana umri wa miaka 28 alikuwa anafanya mazoezi mjini Bujumbura baada ya mkataba na Geita Gold kumalizika

Mbali ya Geita Gold amewahi kuzitumkia timu za Vital’ O, Lydia Ludic Academic, Flambeau de l’est za Burundi, SC Villa ya Uganda, Power Dynamos ya Zambia na Kakamega Home Boys ya Kenya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live