Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Golikipa Argentina amjibu Kylian Mbappe

Martinez Vs Mbappe World Cup Golikipa Argentina amjibu Kylian Mbappe

Fri, 7 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Golikipa wa Aston Villa, Emiliano Martínez amemjibu winga mpya wa Real Madrid, Kylian Mbappé baada ya Mfaransa huyo kudai kushinda Euro ni kugumu zaidi ya kushinda kombe la Dunia.

Martinez (31) ambaye aliiongoza Argentina kutwaa ubingwa wa Dunia mnamo 2022 amesema, “Hakuna kitu kigumu kama kushinda kombe la Dunia na kila mmoja analijua hilo vizuri sana”

Awali Mbappé alisema “Kwangu mimi kushinda michuano ya Euro kugumu kuliko kombe la Dunia. Ingawa kuna presha kubwa kwenye kombe la Dunia. Hapa Ulaya timu timu nyingi zinajuana, tunakutana mara kwa mara. Kimbinu ni soka la kufanana sana.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live