Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Golikipa Al Ahly alia na figisu za Mamelodi Afrika ya Kusini

Mohamed El Shennawy Golikipa wa klabu ya Al Ahly Mohamed El Shenawy

Sat, 11 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Golikipa wa klabu ya Al Ahly Mohamed El Shenawy ameonyeshwa kutofurahishwa na klabu ya Mamelodi Sundowns kupanga mechi yao ya klabu Bingwa Barani Afrika ichezwe majira ya saa 9.

Mohamed El Shenawy amesema;

"Katika dunia ya sasa sidhani kama kuna sehemu ambayo mechi inapangwa kuchezwa muda huu wa mchana hivi".

"Mechi zote zinapangwa kuchezwa majira ya jioni".

Mechi kati ya Mamelodi Sundowns dhidi ya Al Ahly itachezwa majira ya saa 9 Mchana Afrika ya Kusini Saa 10 hapa Tanzania.

Mwenye mawasiliano ya huyu kipa amfahamishe huku kwetu mechi zinachezwa mpaka saa 7 ama saa 8 mchana bila shida yeyote.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live