Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Goli la dakika za jioni lawapeleka Liverpool juu ya Chelsea

Wolves Liver Furaha ya goli la dakika za lala salama

Sun, 5 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Najua kwa nini Liverpool hawataki kumwachia Origi, Licha ya kutopata nafasi ya kucheza mara kwa mara kunako kikosi hicho cha Majogoo wa Jiji.

Jana Liverpool ilikamatika kweli kweli kusaka goli katika mtanange dhidi ya Wolves pale Molineux Stadium.

Bao la mshambuliaji Mbelgiji mwenye asili ya Kenya aliyetokea benchi, Divock Origi dakika ya 90+4 limeipa Liverpool ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Wolverhampton Wanderers katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Molineux.

Liverpool ya kocha Mjerumani, Jurgen Klopp inafikisha pointi 34 baada ya ushindi huo na kusogea nafasi ya pili, ikizidiwa pointi moja na mabingwa watetezi, Manchester City baada ya wote kucheza mechi 15, na kumshusha kinara aliedumu katika nafasi hiyo kwa wiki kadhaa Chelsea baada ya kukubali kichapo mbele ya West Ham.

Wolves inabaki na pointi zake 21 za mechi 15 ikiwa katika nafasi ya nane katika msimamo wa EPL.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live