Wamiliki hao wa klabu hiyo ya England wanatarajiwa kufuta mpango wa kuuza timu hiyo wakidai kuwa Wawekezaji hawajafikia kiwango cha bei ambacho wanakitaka ili kuiachia klabu, ambapo wao wanataka Pauni Bilioni 10 (Tsh. Trilioni 31.4).
Ikiwa uamuzi huo utafanyika unaweza kuibua hasira za baadhi ya mashabiki wa United ambao wamekuwa wakiamini Familia ya Glazer ni chanzo cha timu yao kutofanya vizuri kutokana na uwekezaji mbovu.
Novemba 2022, Familia ya Glazer iliweka wazi kuwa inatarajia kuiuza Manchester United.
Hadi wakati huu Wawekezaji waliosalia kwenye mchakato ni Sheik Jassim wa Qatar na Sir Jim Ratcliffe wa Uingereza.