Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Glazer wanaamini wataendelea kubaki Man United

Glazerssss Glazer wanaamini wataendelea kubaki Man United

Thu, 20 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Familia ya Glazer ambayo ndio wamiliki wa klabu ya Manchester United inaelezwa wana matumaini makubwa kua klabu hiyo itaendelea kua chini yao na sio kuiuza klabu hiyo kwa wamiliki wengine.

Klabu ya Manchester United ilitangazwa kuwekwa sokoni na wamiliki hao mwishoni mwa mwaka jana lakini Glazers family wanaonekana wanahitaji kubaki ndani ya klabu hiyo na hiyo ni kutoka kwenye vyanzo mbalimbali kutoka nchini Uingereza.

GlazerMan United ilikua inawaniwa na matajiri wa kutoka Qatar wakiongozwa na Sheikh Jassim Bin Hamad Al Thani, pamoja na tajiri wa kiingereza Sir Jim Ratcliff lakini taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo zinaeleza kua wamiliki hao hawana mpango wa kuiuza klabu hiyo tena.

Tajiri kutoka Qatar Sheikh Jassim inaelezwa mpaka wakati huu ndio alikua anaongoza kwa dau kubwa mbele ya tajiri mwingine ambaye alikua anaiwania klabu hiyo Sir Jim Ratcliff wamiliki Glazer wanaamini kua wana uwezo wa kuendelea kuimiliki timu hiyo.

GlazerMashabiki wa klabu ya Manchester United wameipokea vibaya taarifa ya familia ya Glazer kuendelea kuimiliki klabu hiyo, Kwani mashabiki hao wanaamini wamiliki hao ni chanzo cha klabu hiyo kufanya vibaya siku za karibuni na ni kitu ambacho wamekua wakikipinga kwa muda mrefu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: