Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Giroud ajilaumu kwa kadi nyekundu aliyopewa

Olivier Giroud Red Card Giroud alivua jezi yake na kuoneshwa kadi nyekundu baada ya wawli kuoneshwa kadi ya njano

Mon, 7 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa AC Milan Olivier Giroud amejikasirikia yeye mwenyewe baada ya kusahau kuwa tayari alikuwa na kadi ya njano na hivyo baada ya kufunga bao la ushindi dhidi ya Spezia akavua jezi ambayo ilipeleka kupata kadi ya pili ambayo ni nyekundu.

Giroud aliingia akitokea benchi na kuiwezesha timu yake kupata ushindi dakika ya 89 baada ya kupewa assist na Sandro Tonali.

Mshambuliaji huyo wa Ufaransa alipewa kadi ya njano dakika sita kabla ya kufunga bao hilo muhimu kwa Milan.

Giroud amekuwa kwenye kiwango bora wiki iliyopita, akifunga mabao mawili na kutoa pasi nyingi zaidi katika ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Salzburg na kukiweka kikosi hicho cha Stefano Pioli katika hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Mshambuliaji huyo aliiambia Sky Sport kuwa;

“Hakika lilikuwa bao zuri sana, ambalo lilikuja kutokana na pasi ya Tonali, tulitaka kushinda mechi hii, cha muhimu ni kuwa na pointi tatu zaidi kwenye msimamo lakini nina hasira kwa sababu nilisahau kadi ya njano ya kwanza.”

Alisema pia hakufikiria vizuri kutokana na shangwe la kufunga bao hilo la ushindi, na pia kichwani kwake bado ni mtoto, lakini ana imani kubwa na timu na pia Jumanne watapambana dhidi ya Cremonese ili wapate pointi 3.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live