Mshambuliaji wa Ufaransa, Olivier Giroud amefikia rekodi ya Thierry Henry kama mfungaji bora wa wakati wote wa timu ya Taifa Ufaransa akifunga jumla ya mabao 51 tangu aanze kuitumikia timu hiyo.
Giroud ambaye kabla ya jana, alikuwa na magoli 49, amefikia rekodi hiyo baada ya kuifungia Ufaransa magoli mawili dhidi ya Australia.
⚽5️⃣1️⃣ Olivier Giroud ⚽5️⃣1️⃣ Thierry Henry
Ufaransa ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Australia katika mchezo wa Kundi D wa Kombe la Dunia, mabao yaliyofungwa na Adrien Rabiot dakika ya 27, Olivier Giroud dakika ya 32 na 71 na Kyllian Mbappé dakika ya 68 huku Australia wakipata bao lao mapema kabisa kupitia kwa Goodwin dakika ya 9.
Thierry Henry ambaye ameshastaafu kuichezea Timu ya Taifa ya Ufaransa ameichezea michezi 123 na kufunga mabao 51 tangu Oktoba 1997 alipoanza kuitumikia Ufaransa akianza kwa kuwafunga Afrika Kusini katika michuano ya Kombe la Dunia mwaka 1998.
Kabla ya henry, rekodi hiyo ilikuwa ikishikiliwa na ambaye Michel Platini. Henry alifunga bao lake la mwisho wakati Ufaransa ikicheza na Austria katika Fainali za Kombe la Dunia, Oktoba mwaka 2010.
Henry hajawahi ufunga hat-trick katika timu ya Taifa, japo amewahi kufunga mabao mawili mawili katika mechi saba tofauti.