Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Giggy aahidi makubwa Yanga, amtaja Aucho

Gift Gigy Giggy aahidi makubwa Yanga

Wed, 12 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Beki mpya wa Yanga, Gift Fred raia wa Uganda amesema kuwa anayo furaha kubwa kujiunga na timu hiyo kwa kuwa ilikuwa ndoto yake kucheza timu kubwa barani Afrika hivyo ni wakati wake kuonyesha kile alichonacho na kuisaidia timu kufikia malengo yake.

Gift ama Giggy au Vacuum Cleaner Waganda wanapenda kumuita hivyo amesema kuwa amekuwa akiifuatilia yanga tangu zamani na amekuwa akizungumza pia na kiungo wa Yanga, Mganda mwenzake Khalid Aucho ambaye amemfanya iwe rahisi kushawishika kujiunga na Yanga.

“Ninafuraha kujiunga na Yanga, nimekuwa nikiifuatilia Yanga tangu zamani ninajua umhimu wa kuichezea Yanga, ninafahamu pia ni timu yenye mashabiki wengi wenye vibe, ninafurahi kuwa sehemu ya kikosi hiki na ninaahidi nitapambana kuhakikisha tunafikia malengo ya timu.

“Nimeichagua Yanga kwa sababu ni klabu kubwa barani Afrika na miongoni mwa vilabu bora Afrika, kwa hiyo ni ndoto ya kila mchezaji kucheza klabu kubwa kama hii ili kufikia malengo yake.

“Ninafurahi zaidi kucheza kama beki, sijawahi kucheza nafasi nyingine kama starika na sijui lakini lakini ninaweza kufunga pia, kwenye mipira ya adhabu ama kona. Nafahamu msimu huu utakuwa na changamoto nyingi za kupambana ili kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza, lakini nitapambana.

“Kuna changamoto kubwa kucheza Tanzania kwa sababu mashabiki ni wengi na Watanzania wanapenda sana soka ukilinganisha na Uganda, kwa hiyo kila mchezaji analamizimika kucheza kwa kujituma ili kuwapa furaha mashabiki.

“Nimekuwa nikizungumza na Khalid Aucho na hakuwa na maneno mengi ya kuniambia zaidi ya kusema kwa Yanga ninapaswa kujituma sana na kuwa serious, kujitoa kila kitu ili kuhakikisha ninafanya voizuri.

“Nikiwa kule sijafanikiwa kuchukua taji lolote kwa miaka miwili, na hivi karibuni tulipoteza nafasi ya kuchukua ubingwa mechi ya mwisho. Lakini kwa hapa Yanga ni furaha kujijunga kwa sababu imechukua kila kitu msimu uliopita na ni wakati sasa wa kupambana kutetea mataji hayo na ikiwezekana kupata tuzo yangu kwa mapenzi ya mungu.

“Ni hatua kubwa kujiunga Yanga, ni wakati sasa wa kujikuza zaidi na kuwa mchezaji mkubwa ndani na nje ya Tanzania na Afrika kwa ujumla, kwa kusaidiana na wenzangu kwenye timu naamini tutafanikiwa. Daima mbele nyuma mwiko,” amesema Gift.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live