Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gift ni zawadi ya Nabi kwa Gamondi

Gift Fred 2024 03 26T132321 Gift ni zawadi ya Nabi kwa Gamondi

Wed, 17 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati Kocha Nssredine Nabi anawasilisha ripoti yake kuhusu kikosi chake, ndani yake lilikuwepo pendekezo la kuongezewa beki wa kati mmoja ili kutanua wigo wa kikosi chake pamoja kuboresha safu ya ulinzi.

Kama kawaida ambavyo Mimi na wewe hatumjui scouting wa Yanga, ndiyo ulikuwa wakati wa Eng. Heris Said kumpelekea Nabi jina la Gift Fred mezani kwake.

Naye bila ajizi kama ilivyo ada yake kuhusu falsafa zake za kiulinzi kwa mlinzi ni uwezo wa kupokea, kumiliki mpira na kuanzisha mashambulizi kuanzia eneo la ulinzi.

Nabi kafungua rejea yake kumfuatilia Gift Fred ni nani pamoja na kujiridhisha wazungu wamo, hawamo? Ndipo akajiridhisha na kugundua yaliyomo yamo, akapitisha jina lake, sura ya kazi ikatia kandarasi ya miaka 3 katika viunga vya Jangwani.

Moja ya kauli za Javier Mascherano kwenda kwa wachezaji wenzake ni kuwa: "Unapopewa jukumu la kufanya uwanjani hata kama wewe hujawahi fanya usikatae, jaribu kwa sababu kocha wako anaona kuliko wewe na yeye ndio mtaalamu."

Kauli hii alikuja kuiamini baada ya yeye mwenyewe wakati anatua Camp Nou (Barcelona), alikuta nafasi yake ya kiungo mkabaji tayari inajabari Sergio Busquets.

Ndipo siku Moja mwalimu wake Pep Guardiola alimjaribu kumtumia kama mlinzi wa kati, nafasi ambayo alikuja kufanya vizuri zaidi mpaka akaaminiwa, anaamini, kama angeishi kwa kukariri nafasi Moja tu uwanjani basi asingedumu na kuheshimika Barcelona.

Gift ni Mali, Gift ni zawadi aliyoachiwa Miguel Angel Gamond, ambaye nae amekuja kutukumbusha ile stori ya Pep Guardiola na Javier Mascherano.

Kumbe Gift Fred ni Versatile player ambaye hatukuwahi kujua, utulivu, akili, uwezo wa kukokota mpira na kupiga pasi sahihi katika mazingira yoyote (Pasi fupi na ndefu) ni talanta aliyonayo kuhusu mpira.

Kama Kuna mtu aliandaa mkeka wake akaorodhesha na jina lake ili kumpunguza kikosini, basi namuona Gift Fred akienda kuchana mkeka huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live