Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gift Fredy apewa nafasi nyingine Yanga

Gift Fred Gd Gift Fredy apewa nafasi nyingine Yanga

Wed, 24 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mlinzi wa kati wa Timu ya Yanga, Gift Fred raia wa Uganda amepewa nafasi nyingine ya kupigarnia nafasi yake katika kikosi cha kwanza.

Gift aliyetua Yanga katika dirisha kubwa la usajili lililopita akitokea SC Villa ya Uganda, alimanusra apewe mkono Wa kwaheri katika usajili wa dirisha dogo.

Hata hivyo kiwango alichoonyesha katika michuano ya kombe la Mapinduzi kikabadili upepo kwani Kocha Miguel Gamondi akapendekeza Mganda huyo aendelee kusalia katika kikosi chake.

Ni wazi bado atakuwa na kazi ya kupigania nafasi yake mbele ya nahodha Bakari Nondo Mwamnyeto, Ibrahim Bacca na Dickson Job wakati yeye akiendelea na mazoezi Avic Town, wenzake wako kwenye majukumu ya timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars' wakishiriki michuano ya Afcon 2023.

Hatma ya Tanzania kuendelea kubaki Ivory Coast au kurejea nchini itaamuliwa leo kwenye mchezo wa tatu hatua ya makundi dhidi ya DR Congo. Tanzania inahitaji kushinda mchezo huo ili kukata tiketi ya hatua ya mtoano.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live