Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gift Fred ilikuwa suala la muda tu Yanga

Gift Fred Gd Gift Fredy.

Wed, 14 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Beki wa Yanga, Gift Fredy amesema lilikuwa ni suala la muda kwake kupata nafasi ya kucheza na kutokukata tamaa ndiyo siri ya mafanikio anayoyapata sasa.

Beki huyo ameliambia Mwanaspoti, sio rahisi kupata nafasi ya kucheza kwenye timu kubwa ambayo tayari kila mchezaji amejitengenezea ufalme eneo lake.

"Nimetua timu ambayo ina wachezaji wengi, eneo ninalocheza kuna watu na tayari wamejenga uaminifu kwa kocha, lakini nilikuwa nahitaji muda zaidi ili kuingia kwenye mfumo;

"Sikukata tamaa, niliamini ipo siku nitacheza kwa kuanza kuonyesha uwezo kwenye uwanja wa mazoezi ili kumshawishi kocha anipe nafasi na sasa muda umefika," alisema.

Gift amesema amewakuta Bakari Mwamnyeto, Dickos Job na Ibrahim Hamad 'Bacca' wakiwa na misimu miwili mizuri nyuma, hivyo alikuwa na kazi ngumu ya kufanya na kujifunza kutoka kwao ili aweze kuingia kwenye mfumo na kufahamu namna timu inataka kucheza.

Akizungumzia dakika chache alizopata dhidi ya Tanzania Prisons akiingia kuchukua nafasi ya Pacome Zouzoua, Gift amesema Kocha Miguel Gamondi alimpa kazi moja tu ya kufanya akiingia.

"Kocha aliniambia ananiingiza kwenda kulinda ushindi wetu tulioupata kipindi cha kwanza, nisifanye kosa lolote tunahitaji pointi tatu muhimu;

"Mchezo ulikuwa mzuri kipindi cha kwanza kwa sababu ulikuwa upande wetu, lakini mara baada ya kucheza tukiwa pungufu baada ya kipa Metacha Mnata kutolewa, tulizidiwa na ndipo kocha akanipa nafasi ya kuingia ili niende kulinda ushindi hilo lilifanikiwa," alisema.

Amesema kwa sasa wana kazi kubwa ya kufanya kuhakikisha wanatetea taji lao huku akikiri ligi ni ngumu hasa mzunguko wa pili utakaoanza baada ya mchezo wao wa mwisho wa mzunguko wa kwanza dhidi ya KMC.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live