Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ghana wachezea kichapo Kombe la Dunia, Ronaldo aweka rekodi

Portugal Vs Ghana Ronaldo alifunga bao la kwanza la Ureno

Fri, 25 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wawakilishi wengine kutoka bara la Afrika timu ya Ghana wameanza michuano ya Kombe la Dunia kwa kupokea kichapo cha mabao 3-2 kutoka kwa Ureno.

Mchezo huo ambao Ureno iliutawala kwa kiasi kikubwa ulishuhudia mabao 5 yakipatikana kipindi cha pili baada ya dakika 45 za kipindi cha kwanza kumalizika pasipo kufungana.

Magoli ya Ureno yalifungwa na C. Ronaldo kwa mkwaju wa penati baada ya kufanyiwa madhambi na mlinzi wa Ghana, lakini Andrew Ayew kusawazisha dakika chache.

Joao Felix na  Leao wakaipatia Ureno mabao ya haraka haraka na kuwavunja nguvu Ghana.

Bukari akaipatia Ghana bao la pili lililowafanya Ghana kupambana angalau watafute sare, lakini mpaka dakika 90 zinakamilika matokeo yakabaki 3-2.

Goli la Cristiano Ronaldo linamfanya kuweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga katika michuano mitano ya Kombe la Dunia tangu aanze kuichezea Ureno.

Ronaldo amecheza michuano ya mwaka 2006, 2010, 2014, 2018 na 2022 na katika michuano yote hiyo amefanikiwa kupachika magoli.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live