Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ghafla Amrabat kawa gumzo AFCON

Sofyan Amrabat Red Card Ghafla Amrabat kawa gumzo AFCON

Thu, 1 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mashabiki wa soka wameanza kumkejeli Sofyan Amrabat baada ya kiungo huyo wa Manchester United kutolewa nje kwa kadi nyekundu mara mbili ndani ya mechi moja wakati taifa lake la Morocco lilipofungashiwa virago kwenye fainali za Afcon 2023 huko Ivory Coast.

Amrabat bado hajatiki mambo yake huko Man United, ambako amejiunga kwa mkopo akitokea Fiorentina ya Serie A kwa thamani ya Pauni 8.5 milioni.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 27 ameanzishwa kwenye mechi saba kati ya 13 alizocheza kwenye Ligi Kuu England, huku Man United ikiwa na ruhusa kumbeba jumla mwisho wa msimu kwa Pauni 21.4 milioni.

Kiungo Amrabat alikosa mechi tatu zilizopita za Man United kwa kuwa yupo kwenye Afcon 2023, lakini kama alidhani hilo lingempa ahueni ya kusahau magumu ya huko Old Trafford, amekosea, majanga kotekote.

Usiku wa juzi Jumanne, Amrabat na chama lake la Morocco lilikomea kwenye hatua ya 16 bora ya fainali za Afcon 2023 baada ya kuchapwa na Afrika Kusini mabao 2-0. Timu namba moja kwenye viwango vya Fifa kwa Bara la Afrika, imefungwa na timu namba 13 kwenye viwango hivyo. Mshtuko mkubwa.

Mambo yalitibuka zaidi kwa Amrabat baada kutolewa kwa kadi nyekundu katika dakika za mwisho za mechi hiyo ya juzi. Amrabat alimwangusha kiungo wa Afrika Kusini, Teboho Mokoena, aliyekuwa akichanja mbuga kuelekea kwenye boksi la Morocco, akaonyeshwa kadi ya pili na njano na kutolewa kwa nyekundu.

Mpira uliopigwa kwenye adhabu hiyo iliwapa Afrika Kusini bao la pili na kujihakikishia ushindi.

Wakati Amrabat anatoka nje, alirudisha uwanjani kwa kuwa mwamuzi alikuwa anakwenda kuthibitisha kwenye VAR, ndipo refa huyo aliporudi na kufuta ile kadi ya njano na kumwonyesha nyekundu ya moja kwa moja kwa sababu ilionekana Amrabat alikuwa beki wa mwisho wakati anamfanyia madhambi Mokoena.

Kitendo cha Amrabat kuonyeshwa kadi nyekundu mara mbili kwenye tukio moja, liliwafanya mashabiki waanza kumdhihaki, ambapo mmoja alisema kwenye mitandao ya kijamii: “Amrabat alitolewa baada ya kadi ya pili ya njano, kisha akaambiwa rudi uwanja kwa ajili ya VAR, baadaye akaonyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja, ni kama sinema vile.”

Mwingine alisema: “Amrabat ni kweli ametolewa kwa kadi nyekundu mbili!” Shabiki mmoja alisema: “Hii Afcon sijawahi kuiona. Ni burudani ya aina yake, yeyote anaweza kushinda.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live