Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Getafe yamtetea Greenwood

Mason Greenwood Hispania Mason Greenwood akiwa mazoezini Getafe

Sat, 9 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Haya sasa. Getafe imetetea uamuzi wa kumsajili Mason Greenwood katika dirisha la usajili la kiangazi, ikidai fowadi huyo wa Manchester United hana tofauti na wachezaji wengine.

Kabla ya Getafe kumsajili Greenwood kwa mkopo alikuwa chini ya uchunguzi wa ndani uliosimamiwa na Man United kabla ya kutoa tamko rasmi kuhusu hatma yake, lakini baada ya miezi sita ya uchunguzi kukamilika uongozi wa klabu uliamua kumtoa Greenwood kwa mkopo akaanze maisha yake mapya nje ya England.

Kutua kwa Greenwood Getafe ilishtua Hispania hususan taasisi za kijamii huku wakiishutumu kutokana na uamuzi wao kabla ya utambulisho wake Jumatano iliyopita.

Hata hivyo, uongozi wa Getafe ulimkingia kifua kutokana na uamuzi wao wa kumleta mchezaji huyo wa kimataifa wa England ili kuimarisha safu yao ya ushambuliaji.

“Tulifanya kile tulichofanya, Tulimsajili Greenwood kwa sababu kulikuwa hakuna kizuizi,” alisema Mkurugenzi wa michezo wa Getafe, Ruben Reyes. “Tumemsajili Greewood kama tulivyowasajili wachezaji wengine (Diego Rico na Oscar Rodriguez). Tulipaswa kufanya kazi yetu na hilo ndilo tulizingatia.”

Ripoti ziliripoti Man United iliweka kipengele cha kuvunja mkataba wa mkopo itakapofika dirisha dogo la usajili Januari hivyo kuna uwezekano akarudi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live