Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gerrard amtaka Coutinho Villa Park

Philippe Coutinho Philipe Coutinho

Wed, 5 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa klabu ya Aston Villa Steven Gerrard yupo kwenye mazungumzo na klabu ya Barcelona ili kuweza kumchukua kiungo Philippe Coutinho kwa mkopo wa miezi sita.

Philippe Coutinho ameshawai kucheza timu moja na kocha huyo katika klabu ya Liverpool kwa muda wa miaka miwili, Steven Gerrard pia anavutiwa na kiungo ambaye hapewi nafasi ya kutosha kwenye klabu ya Barcelona licha uwepo wa kocha mpya kwenye klabu hiyo.

Coutinho hajaweza kumshawishi kocha wake kiasi kwamba ameshindwa kupata nafasi kama wanazopata Gavi, Nico Gonzalez, Frenkie de Jong na Pedri kwenye kikosi cha Barcelona.

Barcelona kwa sasa wapo katika hali mbaya ya kiuchimi huku wakiwa na mipango ya kupunguza hati za malipo ya mishahara, ili waweze kuwasajiri wachezaji wapya ambao wamewanunu hivi karibuni kwenye timu ya wakubwa ambao ni Ferran Torres na Dani Alves.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live