Tangu kuanza kwa Msimu mpya EPL 2021/2022 Kikosi cha Aston Villa chini ya Mwalimu wao Dean Smith hawakua na matokeo ya kuridhisha.
Hali ilikua mbaya zaidi mwezi Oktoba ambapo walipoteza michezo mitano mfululizo na kumtimua kocha wao Dean Smith, Kisha kibarua akapewa Nahodha wa zamani wa Liverpool Steven Gerrard ambae alikuwa na Kikosi cha Rangers.
Gerrard amesaini mkataba wa miaka mitatu na nusu, na tangu atue kikosini hapo amecheza michezo minne na amepoteza mmoja tu chini ya Pep Guardiola.
Jana Jumapili ameshinda mbele ya Meneja wake wa zamani Brendan Rodgers, akiitandika Leicester City magoli 2-1.
Magoli ya Villa yamefungwa na beki wao wa kati, E Konsa Ngoyo (17' 54') wakati lile la Leicester likifungwa na H Barnes (14').
Gerrard atarudi anfield Disemba 11 kuvaana na Liverpool klabu ya ndoto yake na maisha yake ambako amedumu kwa zaidi ya muongo mmoja katika viunga vya Anfield.
Je ataweza kuhimili shughuli pevu ya majogoo hao wa Jiji?