Magwiji kutoka katika vilabu viwili vya soka nchini England, liverpool n Chelsea huenda wakarejea kufundisha soka nchini humo siku chache zijazo.
Steven Gerrard na Frank Lampard, wanahusishwa na kuvinoa vilabu vya Norwich City na Aston Villa ambavyo vimefukuza makocha wake hivi karibuni.
Norwich wao walimfungashia virago Daniel Farke, wakati Aston Villa wao walimtimua Dean Smith, kutokana na matokeo mabaya ya timu hizo.
Lampard kwa sasa hana kazi baada ya kutimuliwa Chelsea wakati Gerrard yeye anakinoa kikosi cha Rangers.
Katika msimamo wa EPL, Norwich inakamata nafasi ya mwisho ikiwa na alama tano, baada ya kushuka dimbani michezo 11.
Aston Villa wao wanakamata nafasi ya 16 wakiwa na alama 10 wakiwa wamecheza michezo 11.