Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gerard Pique auota Urais Barcelona

Gerrard Pique GG Gerard Pique

Thu, 10 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliekua beki wa klabu ya Barcelona na timu ya taifa ya Hispania ambae amestaafu hivi karibuni Gerard pique amezungumzia juu ya suala la yeye kuja kua Rais wa klabu hiyo siku zijazo.

Beki huyo ambae aliagwa katika dimba la Camp Nou wikiendi iliyopita, ameweka wazi azma yake ya kuja kuiongoza klabu hiyo ya maisha yake ambayo ameitumikia kwa takribani miaka 14 kabla ya kuamua kustaafu.

Pique ameondoka ndani ya klabu ya Barcelona baada ya kuitumikia kwa miaka 14 na kuisaidia kushinda kila taji kwenye ngazi ya klabu ikiwemo La liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya,Spanish super Cup pamoja klabu bingwa ya dunia ikiwa ni baadhi ya mataji ambayo amebeba klabuni hapo.

Beki huyo anafikiria kuja kuiongoza klabu hiyo siku moja lakini kwasasa atafanya mambo mengine baada ya kustaafu na hiyo inaweza kua siku za baadae.

Beki Pique pia amewahi kuitumikia klabu ya Manchester United na kufanikiwa kubeba mataji ya ligi kuu ya Uingereza mawili pamoja na ligi ya mabingwa ulaya mwaka 2008.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live