Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gerald Mdamu; Maana halisi ya kipaji na tafsri ya kabla hujafa hujaumbika

GERALD Mdamu Gerald Mdamu.

Fri, 17 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenyezi Mungu baada ya kufanya uumbaji kila mtu alimajia kipaji chake, Ambacho huwa tofauti baina ya mtu mmoja na mwingine.

Ni kweli kila mtu hubarikiwa kipaji lakini kukiendeleza na kukitumia kipaji ni jambo lingine, Kwa maana ukizingatia wapo wengi wenye vipaji vikubwa lakini wanateseka.

Ila nitakwambia kitu kuhusu Gerald Mathias Mdamu na baraka ya kipaji cha mpira kisha kukitumia na kukiendeleza ipasavyo.

Gerald Mdamu ni miongoni mwa vijana Wakitanzania waliobarikiwa maarifa na uwezo mkubwa wa kuufanyia chochote mpira wa miguu na ukatii mithili ya wanafanzi na kutii kengele.

Takwambia Mdamu alikuwa kipenzi cha mashabiki wa mpira sio kwa bahati mbaya ni kutokana na uwwzo wake wa kuchezea mpira. Kuanzia pale Shinyanga, Mara mpaka Moshi kamwe hawawezi kusahau zile ladha za mpira kutoka kwa Mdamu.

Sikuwahi kuwa mpenzi wa misemo ya wahenga lakini katika mitihani nilikuwa mpenzi wa kujibu maswali kuhusiana na misemo "wahenga".

Kiukweli wahenga wanazo kauli nyingi sana lakini vijana wa leo wanasema hata muhenga mwenyewe na mdharau na chochote hakinipati.

Lakini wacha nikwambie kitu kuhusu wahenga waliposema kuwa "Kabla ujafa haujaumbika". Dah Aise ila walikuwa na maana kubwa sana.

Wakati unatembea ukiwa mzima wa afya kabisa kumbuka kuwa changamoto zinaweza kukuta muda wowote ule na ndicho kitu kilimkuta Gerald Mdamu.

Ilikuwa vigumu sana kufikiria kuwa Mdamu katika maisha yake mbeleni angekosa kabisa uwezo wa kucheza mpira, Lakini kwakuwa ni binadamu na Mungu kapanga basi imekuwa ivo.

Gerald Mdamu Kipaji kikubwa sana cha mpira, Foward katili sana mbele ya lango na kipenzi cha mashabiki halisi wa mpira leo hata kupiga danadana mpira hawezi tena. Respect wahenga.

Endelea kuugua pole fundi wa mpira Mdamu but wito wangu kwa wadau kama una chochote samahani sana nenda kampe Sapoti Mdamu anapitia Mengi sana Magumu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live