Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

George Mpole azua taharuki Geita Gold

George Mpole Agoma George Mpole

Fri, 4 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji nyota na kinara wa mabao wa Ligi Kuu msimu uliopita, George Mpole inadaiwa amelizua baada ya kujiengua ndani ya kikosi hicho kwa kilichoelezwa kushinikizwa alipwe fedha anazoidai klabu hiyo.

Mpole aliyefunga mabao 17 na kukeba kiatu cha dhahabu mbele ya straika wa Yanga, Fiston Mayele aliyefunga 16, ameshindwa kucheza michezo mitatu iliyopita ya timu hiyo ukiwamo ule wa Yanga uliopigwa CCM Kirumba, jijini Mwanza na wageni kushinda bao 1-0.

Habari za ndani ya timu hiyo zilisema Mpole alijiwekwa kando ili kushinikizwa kulipwa fedha zake zote ikiwamo mshahara wa kuanzia Septemba, japokuwa mabosi wa klabu hiyo wameeleza nyota ana matatizo ya kifamilia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live