Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

George: Leo una hojiwa uzalendo wa Dickson Job?

Jemedari X Job Dickson Job.

Fri, 15 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

George Job ambaye ni Meneja wa beki wa kati wa Yanga na Timu ya Taifa ya Tanzania, Dickson Job amewavaa baadhi ya wachambuzi wanaodai kuwa mchezaji huyo ameonekana kuwa msaliti na kukosa uzalendo kwa Taifa lake.

Kauli hiyo ya George inakuja baada ya Kocha wa Taifa Stars, Hemed Morocco kumpiga chini Job kwenye Timu ya Taifa huku chanzo kikidaiwa kuwa ni utovu wa nidhamu akiwa AFCON kwa kugomea kucheza beki namba 2.

"Katumikia taifa tangu akiwa na miaka 16, leo una hojiwa uzalendo wake? Kishacheza na maumivu leo kawa msaliti?

"Mechi 4 kati ya 6 za kufuzu kacheza namba 2, kwanini isiwe mechi na Congo? Mechi kubwa na muhimu kwa taifa," amesema George Job.

Je, Job ni msaliti?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live