Wed, 8 Mar 2023
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Wakati maneno yakiwa ni mengi kuhusiana na kiwango cha Simba SC katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika.
Mchambuzi wa michezo kutoka kipindi cha Sports Arena ya Wasafi FM amekwenda mbali na kutoa hitimisho la kiwango cha Simba kama kitaendelea kwa namna ilivyo sasa.
Simba SC wanajiandaa na mchezo dhidi ya Horoya kutoka Guinea Machi 18 katika Uwanja wa Mkapa.
Sasa kuelekea mchezo huo Job anasema;
“Horoya akija kwa Mkapa na Simba akacheza kama alivyocheza na Vipers basi it’s Over kwa Simba.”
Simba imeshinda michezo miwili kati ya minne iliyokwishacheza katika hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Afrika.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live