Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

George Job: Impact ya Saido Kimataifa ni ndogo sana

Saido X Job Saido

Thu, 27 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati Simba SC ikijiandaa kuikabili Wydad mchezo wa mkondo wa pili wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kiungo mshambuliaji wa Timu hiyo Saido Ntibazonkiza anaonekana kutokuwa na makali katika michezo ya Kimataifa jambo linalozungumzwa kuwa mwalimu angeangalia mtu mwingine wa kuanza katika nafasi yake.

Akizungumza mchambuzi wa Michezo George Job anasema;

“Ukiangalia impact ya Saido kwenye mechi za kimataifa ni ndogo kulingana na kwenye Ligi, moja kati ya poor performance aliyokuwa nayo Saido ni mchezo uliopita dhidi ya Wydad, huwa anajaribu sana kufanya vitu vitokee lakini ni kama kuna kasi fulani inamuacha tofauti na kwenye ligi, akiwa kwenye Ligi impact yake ni kubwa Hakuna wa kupinga,”

Saido ana magoli 10 na assist 9 Ligi Kuu NBC, huku akiwa ndio mchezaji aliehusika katika magoli mengi kuliko mchezaji yoyote Ligi Kuu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live