Wakati wengi wakilalamikia kiwango cha Nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Ally Samatta anaekipiga nchini Ubelgiji katika klabu ya Genk kuwa haoneshi bidii anapokuwa katika majukumu ya Timu ya Taifa.
Mchambuzi wa Soka kutoka kituo cha Wasafi FM, George Ambangile amemtetea mchezaji huyo huku akionesha kuwa anafanya majukumu zaidi ya mchezaji wa kawaida.
Akuzungumza Ambangile amesema;
"Wengi wanamlalamikia Samatta akiwa Stars ila hawajui kuwa Samatta anapokuwa Uwanjani huwa anafanya kazi za watu wawili.Kushuka chini kuiunganisha timu na wakati huo huo anapaswa kuwa eneo la umaliziaji.Sababu ya yote hii ni vile sisi hatuna kina Chama na Saido"
Samatta ataiongoza Taifa Stars kusaka tiketi dhidi ya Uganda mchezo utakaopigwa kesho Jumanne katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.