Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Geoff Leah amponda Robertinho

Robertinho Mipango Geoff Leah amponda Robertinho

Wed, 8 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa soka Geoff Leah kupitia EFM Radio, amesema kuwa kauli ya aliyekuwa Kocha wa ni uongo na haipaswi kusemwa na kocha mkubwa kama yule kwani ni kisingizio ambacho hakina maana.

Robertinho alidai kuwa kipigo cha bao 5-1 kutoka kwa watani zao Yanga ni kutokana na mshambuliaji wake, Kibu Denis kuumia katikati ya mchezo.

Tayari Robertinho ameshatimuliwa na timu yake ya Simba kutokana na matokeo hayo mabovu.

"Kama kweli Robertinho amesema moja kati ya sababu ya Simba kufungwa juzi ni kuumia kwa Kibu Dennis, basi binafsi yangu sioni kama hilo ni jibu sahihi kutolewa kwa kocha. Inamaana uwepo wake uwanjani ndiyo unaifanya timu iwe bora?

"Ukichunguza kwa mechi mfululizo kikosi cha Simba kinachoanza ndicho kilekile, kimeanza kwenye mechi mfululizo bila mabadiliko, unataka kusema uwepo wa Kibu Dennis ndiyo unaleta maelewano mazuri kwa Inonga na Che Malone? Sioni kama Robertinho ametoa jibu sahihi," amesema Geoff Leah.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live