Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Geoff Leah: Yanga hawana sababu ya kumkumbuka Mayele

Geof Lea X Kokoni Geoff Lea amewazungumzia washambuliaji waliopo hivi sasa Yanga

Sat, 19 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati Yanga wakiwa katika maandalizi ya kujiandaa na mchezo wao wa Hatua ya awali dhidi ya Klabu ya ASAS Djibout.

Mashabiki na wapenzi wengi wa Klabu hiyo wameonekana kuwa na wasiwasi na safu ya ushambuliaji ya Timu hiyo na hasa baada ya kuondoka kwa straika wao hatari Fiston Mayele.

Sasa mchambuzi wa Michezo kutoka EFM, Geoff Leah amewataka Yanga kutokuwa na mashaka na safu ya ushambuliaji iliyopo hivi sasa.

Geoff anasema;

“Wana Yanga wanapaswa watulie kwani inawezekana uwepo wa Musonda, Mzize na Hafiz wanaweza kukifanya zaidi ya kile alichokifanya Mayele kwa Msimu uliopita ”

Yanaga wanaanza kutupa karata yao ya kwanza katika Michuano ya Ligi ya Mabingwa msimuu huu kesho Jumapili dhidi ya ASAS Djibout mchezo wa hatua ya awali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: