Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Geoff Lea awang'ata sikio TFF kuhusu hili

Geoff X Amrouche Geoff Lea awang'ata sikio TFF kuhusu hili

Thu, 14 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa masuala ya soka kupitia EFM Radio, Geofrey Lea amesema kuwa Shirikisho la Tanzania (TFF) linapaswa kulegeza masharti na ada ni kuwavutia wadau wengi wa soka kujifunza masuala ya ukocha wa mpira wa miguu.

Geoff amesema hayo akieleza kuwa, kwa kufanya hivyo kutawahamasisha watu wengi kulijua soka na faida zake hivyo itakuwa rahisi kuwa makocha wengi, wachezaji wengi na kuinua timu ya taoifa ya Tanzania (Taisa Stars).

Kauli hii ya Geoff inakuja ikiwa ni siku chache baada ya Taifa Stars kufanikiwa kutinga Fainali za AFCON 2023 baada ya kutoa sare na Algeria.

"Miaka ya 2000 wakati Ujerumani wanatolewa kwenye michuano ya Euro, taifa zima la Ujerumani likafikia maamuzi ya kufanya mabadiliko kwenye soka lao."

"Kwanza wakagundua kwamba hawatoi nafasi kwa wachezaji ambao ni wahamiaji ndani ya nchi yao, lakini pia wakapunguza ada ya kozi za ukocha na kuwapa nafasi watu wengi kushawishika kujifunza kanuni na mipango ya ukocha mpaka kwa wazazi wao ikawa mpaka wazazi wanahamasishwa kujifunza ukocha ambapo hiyo ikapelekea wazazi wengi kuhamasisha watoto wao kucheza soka.

"Lakini jambo la kushangaza, leo tunajadili kuhusu uraia pacha na kuacha vitu vya msingi kama suala hili la ukocha. Tanzania tuna makocha wachache na hilo tunatakiwa kuliweka sawa," amesema Geoff Lea.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: