Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Geoff Lea: Yanga hawezi kuchukua makombe yote

Yanga Mapinduzi Fg Geoff Lea: Yanga hawezi kuchukua makombe yote

Tue, 9 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa masuala ya soka kutoa EFM, Geoff Lea amesema kuwa Klabu ya Yanga hawawezi kuchukua mataji yote msimu huu hivyo kwani hata timu nyingine zinayataka mataji hayo.

Geoff amesema hayo wakati akiizungumzia Yanga baada ya kutolewa kwenye michuano ya Mapinduzi Cup 2024 katika hatua ya robo fainali kwa kufungwa magoli 3-1 dhidi ya APR ya Rwanda.

“Ukweli wa soka ni kwamba huwezi kuwa na kipaumbele cha kutaka kushinda mataji yote, kwa hiyo, hiyo ni kawaida kwenye soka. Kocha kusema alienda kwenye Mapinduzi Cup akiwa hana mipango ya kushinda michuano hiyo ni kawaida.

“Wachezaji nao ni wana damu hawawezi kupambana kwa asilimia zote kwenye michezo ya michuano yote. Mimi kama kocha ninajua huwezi kuzungumza kila kitu, unatakiwa kuheshimu michuano yote unayoshiriki.

“Hata kwa ile mechi ambayo Yanga ilichezesha wachezaji nane vijana, pale hatusemi vijana bali tunasema Yanga ndiyo imecheza, wote ni wachezaji wa kulipwa na wanafaa kutumika,” amesema mchambuzi Geoff Lea.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live