Mchambuzi wa masuala ya soka kutoka Kiuto cha radio cha EFM Radio, Geoffrey Lea amesema kuwa atakuwa mtu wa mwisho kuamini kwamba Klabu ya Simba ni mbovu kwa msimu huu kutokana na kiwango ambacho wameanza kukionyesha mwanzoni mwa msimu.
Geoff amesema wanaosema Simba si bora waipe muda, itafanya vizuri na itawashangaza wengi.
Kauli hizo zimekuja baada ya wapinzania wao, Yanga SC kuonekana wanafanya vizuri zaidi kuliko Simba kwa mechi za awali ambazo zimeshapigwa mpaka sasa.
"Nadhani mashabiki wa Simba SC hawajaridhishwa na kiwango cha timu yao ingawa nami ni shabiki wa Simba, lakini sipo kwenye kundi hilo kwa sababu naamini huu ni mwanzo wa Ligi
"Kazi aliofanya kocha kwenye mechi ya kujiandaa na msimu haiwezi kuonekana kwenye mechi za mwanzoni kama hizi za mpaka sasa kwahiyo bado naamini kuna kitu kitaonekana lakini lakini yote kwa yoto nafasi ya Simba SC kumtoa Al Ahly ni Ngumu sana," amesema Geaff Leah Via EFM Radio