Mchambuzi wa masuala ya soka Geoff Lea kupitia EFM amesema Klabu ya Young Africans inahitaji mshambuliaji ambaye ataweza kuifanya kazi kama aliyokuwa akiifanya Fiston Mayele msimu uliopita.
Geoff amesema hayo mara baada ya Yanga kucheza michezo mitatu ya ligi ya Mabingwa Afrika bila kupata ushindi wowote huku wakipata sare mechi mbili na kupoteza mmoja.
"Kwanini Yanga hawatengenezi nafasi nyingi, kwanza ni quality of positioning ambapo Yanga wamekuwa wakicheza soka la kumiliki mpira kwa kiasi kikubwa na kufanya timu pinzani kuchagua kubaki nyuma hivyo kuifanya timu pinzani kutoruhusu kutengenezewa nafasi sababu wamekuwa wakibaki nyuma kwa wingi.
"Lakini pia sababu nyingine ni kumkosa Fiston Kalala Mayele, Mayele amekuwa akiwa mshambuliaji aliyefanya makubwa sana kwa msimu uliopita na aliisaidia Yanga sana kwenye hii michuano ya kimataifa hivyo kumkosa mchezaji wa kariba yake ni tatizo kubwa kwa Yanga kuendana na kasi haswa michezo hii ya kimataifa," amesema Geoff Leah.