Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Geof Lea: Kweli timu bora imefungwa na timu ya hamasa

Simba Yanga Baooo.jpeg Simba vs Yanga

Mon, 17 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa masuala ya Soka nchini kupitia kituo cha radio cha EFM, Geof Lea amekiri kuwa ni kweli timu ya Yanga ikiwa bora msimu huu imefungwa na Simba ambayo haiku vizuri sana.

Geof Lea amesema hayo kufuatia kauli ya aliyewahi kuwa Samuel Lukumayambaye aliwahi kuwa kaimu Mwenyekiti wa Yanga baada ya Yanga kufungwa bao 2-0 na watani zao Simba katika Dimba la Mkapa jana Jumapili Aprili 16, 2023.

“Ni kweli timu bora imefungwa na timu ya hamasa. Inafahamika kwamba Yanga ndiyo timu bora hapa nchini kwa sasa, kwanza ni mabingwa watetezi na wanaongoza Ligi. Kufungwa jana hakuzuii mapambano yao ya kusaka ubingwa mwaka huu.

“Kule Uingereza, Liverpool iliifunga Manchester United bao 7-0, lakini Liverpool ipo nyuma kwenye msimamo wa EPL ikilinganishwa na Man United. Ubora wakati mwingine unaweza ni wa jumla (general) au kutokana na siku husika ya mchezo.

“Ukiangalia mwenendo wa mchezo, umiliki wa Yanga ulikuja kipindi cha pili baada ya Simba kuwa wameshawaadhibu Yanga na hawana cha kupoteza kwa dakika zile lakini yanga hawaku-control mchezo wala kutengeneza nafasi.

“Kitu cha kwanza kwenye mchezo ni kufunga wala sio kumiliki, takwimu hizo zipo tu lakini kikubwa ni matokeo na kuondoka na alama tatu muhimu,” amesema Geof Lea.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: