Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Geita yawashtukia Yondani, Nashon

Geita, Kelvin Vs Nashon Kelvin Yondani na Kelvin Nashon

Sat, 4 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uongozi wa klabu ya Geita Gold imewashtukia nyota wake, Kelvin Yondani na Kelvin Nashoni na fasta kukaa nao mezani kwa nia ya kutaka kuwaongezea mikataba mipya.

Mastaa hao mikataba yao ya sasa ipo ukingoni na kuna tetesi kwamba Nashoni anamezewa mate na klabu za Simba na Yanga, hivyo kuwafanya mabosi hao kufanya maamuzi hayo sambamba na kwa Yondani ili kuendelea kuwamiliki.

Akizungumza Mwenyekiti wa Geita Gold, Constantine Moland alisema kwasasa wanapambana kuhakikisha wanamaliza nafasai nne za juu ili wapate nafasi ya kuiwakilisha nchi kimataifa hivyo hawana sababu ya kupoteza kikosi kazi chao.

“Kelvin na Nashon ni moja ya wachezaji ambao wameibeba Geita Gold na uzoefu wao kwenye ligi uliongeza kitu ndani ya timu baada ya kupata saini zao tumeshaanza mazungumzo nao kwaajili ya mikataba mipya hakuna mchezaji ambaye ataondoka kama kocha kapendekeza aongezwe mkataba,” alisema na kuongeza;

“Kikosi chetu tunakiamini na ni bora kutokana na juhudi wananazozifanya sio hao tu ni wachezaji wengi hawana mikataba na kocha kaonyesha nia ya kuendelea nao tutawabakiza kwaajili ya kuipambania timu hadi mwisho wa msimu tutakuwa tumeshamalizana nao.” alisema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live