Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Geita yapangua sita, wawili mara ya kwanza

Geita Goldy Geita yapangua sita, wawili mara ya kwanza

Sat, 7 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Kipa namba moja wa Geita Gold, Erick Johora aliyejiunga na timu hiyo msimu huu akitokea Yanga, leo ameanzia benchi, kumpisha kipa mwenzake, Sebusebu Samson ambaye hajadaka mchezo wowote wa Ligi Kuu Bara msimu huu wakati kikosi hicho kikiikabili Yanga kwenye Uwanja wa CCm Kirumba.

Johora aliyedaka mechi zote nne za Geita, ikiwemo waliopoteza kwa KMC kwa mabao 2-1 likiwamo la kwanza lililotokana na uzembe ni kati ya wachezaji sita waliotemwa kikosi cha kwanza kilichocheza mechi hiyo ikliyopita iliyopigwa Uwanja wa Nyankumbu ili kuikabili Yanga jioni hii.

Kocha Mkuu wa Geita, Hemed Suleiman 'Morocco' amewapiga chini watano wengine akiwamo Raymond Masota, Mligo Antony, Carlos Protas, Godfrey Raphael na Valentino Mashaka.

Beki Erick Kyaruzi naye leo anaanza kwa mara ya kwanza msimu huu kama Sebusebu baada ya kukalia benchi muda mrefu tangu alipojiunga na timu hiyo dirisha dogo la msimu uliopita.

Kikosi cha leo cha Geita Gold: Sebusebu Samson, Mwaita Gereza, Mwankemwa, Kelvin Yondani, Erick Kyaruzi, Samwel Onditi, Godfrey Julius, Tariq Simba, Elias Maguli, Seif Kiakala na George Sangija.

Wachezaji wa akiba ni: Erick Johora, Steven, Godfrey Raphael , Abeid Athuman, Seleman, Yusuph Dunia, Valentino Mashaka na Raymond Masota

Chanzo: Mwanaspoti