Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Geita yamvizia fundi wa Yanga

Hemed Morocco Kocha Geita yamvizia fundi wa Yanga

Mon, 17 Jul 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Wakati Geita Gold ikiendelea na mazungumzo ya kumpata Hemed Suleiman 'Morocco' akakinoe kikosi hicho msimu ujao, tayari viongozi wa timu hiyo wameanza kumpigia hesabu nyota wa zamani wa Yanga, Salvatory Edward 'Doctor' ili akasaidiane naye.

Mazungumzo kati ya Geita na Morocco yanaendelea vizuri na muda wowote atatambulishwa ndani ya kikosi hicho ili kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Fred Felix 'Minziro' aliyesaini dili la mwaka mmoja na maafande wa Tanzania Prisons.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Geita, Simon Shija aliliambia Mwanaspoti kuwa, muda wowote kuanzia sasa watatangaza kocha mpya na msaidizi wake.

"Tumekuwa kwenye vikao kwa muda mrefu lakini kama waswahili wanavyosema kimya kingi kina mshindo, hivyo tutaanza na kocha na baada ya hapo tutaanza kutangaza wachezaji wapya ambao watakuwa sehemu ya kikosi chetu msimu ujao," alisema Shija.

Shija alifafanua sababu kubwa ya kuchelewa kuweka wazi benchi la ufundi ni kufanya tathmini ya kina kwa wale wote walioomba kwani wanahitaji kocha mzuri mwenye kiu ya mafanikio atakayeweza kuendana na ushindani uliopo kwa msimu ujao.

Mazungumzo ya Morocco na Geita yameingia wiki ya pili sasa ila taarifa ambazo Mwanaspoti imezipata kocha huyo amekubali dili la kujiunga nao kwa mkataba wa mwaka mmoja na kuamua kuachana na mabingwa wa Zanzibar, KMKM aliokuwa akiinoa na kuipa taji la msimu wa tatu mfululizo. Baada ya Morocco kuonekana ana nafasi kubwa ndipo viongozi wakahamishia nguvu kumpata Salvatory Edward ili awe msaidizi wake.

Salvatory aliyekuwa akiinoa timu ya taifa ya Walemavu iliyoshiriki Fainali za Kombe la Dunia 2022 enzi za uchezaji wake aliosifika kwa umahiri eneo la kiungo kiasi cha kubatiozwa jina la Dokta.

Mbali na Yanga Edward amewahi kukipiga pia Mtibwa Sugar na Temeka United iliyokuwa ikimilikiwa na aliyekuwa Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu sammba na nyota wengine wa zamani akiwa kipa Kelvin Mhagama na Abuu Ntiro waliowahi kuwika na Simba, Yanga na Taifa Stars.

Chanzo: Mwanaspoti