Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Geita yamnyatia Mmarekani

Geita Gold A0004 Geita yamnyatia Mmarekani

Mon, 13 Nov 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Klabu ya Geita Gold imeanza rasmi mazungumzo ya kumnasa Kocha Mkuu wa Dodoma Jiji, Mmarekani, Melis Medo kwa ajili ya kukiongoza kikosi hicho kutokana na kutoridhishwa na mwenendo wa Kocha, Hemed Suleiman ‘Morocco’ msimu huu.

Taarifa za kuaminika kutoka ndani ya timu hiyo zililiambia Mwanaspoti, viongozi wanataka kufanya mabadiliko ya benchi la ufundi haraka kabla ya mambo hayajakuwa mabaya mbeleni kwani nafasi waliyopo na aina ya uchezaji haiwavutii mabosi.

“Ni kweli mazungumzo yapo lakini hayajafikia sehemu nzuri kwa sababu wamekuwa wakivutana kwenye maslahi hivyo tuendelea kusubiri kwani huenda likatokea kwa sababu ‘Morocco’ mwenyewe yupo tayari kuondoka,” kilisema chanzo hicho.

Kwa upande wa mwenyekiti wa klabu hiyo, Leonard Bugomola alipotafutwa na Mwanaspoti kuzungumzia suala hilo alisema yeye na viongozi wenzake wanatambua kocha wao ni Morocco hivyo hizo habari ndio kwanza anazisikia na hawezi kuzizungumzia.

“Ndugu yangu ndio kwanza unanipa hizo habari kwa sababu mimi sina, bado tuna mkataba na kocha wetu Morocco na hatufanya uamuzi wowote kuhusu yeye, kama itatokea jambo lolote basi tutatoa taarifa rasmi ila kwa hili linaloendelea silijui.”

Wakati Bugomola anazungumza hayo Mwanaspoti linatambua mazungumzo hayo yapo baina ya viongozi wa Geita na kocha huyo kwani hata kwenye kikosi cha Dodoma Jiji alijiweka pembeni, hivyo timu hiyo kusimamiwa na Kocha Msaidizi, Kassim Liogope.

Hadi Ligi Kuu inasimama Geita Gold inashika nafasi ya 15 kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara baada ya kucheza michezo tisa na pointi zake saba kufuatia kushinda mechi moja tu, sare minne na kupoteza pia minne ikiwa juu ya Mtibwa Sugar inayoburuza mkia na pointi tano.

Chanzo: Mwanaspoti